Yanga SC walishinda mechi kipindi cha kwanza na kipindi cha pili wakaingia kuiuwa, kupunguza mwendo wa mchezo, funga spaces katikati ya mistari yao yote mitatu hasa ile miwili ya mwisho halafu ni kama wanawaambia Azam FC "tufungueni kama mnaweza bila nyie kuacha space nyuma yenu). Timu imara ndio inavyocheza
Azam FC kuanza na mabeki watatu nyuma sio kosa bali utekelezaji wake uwanjani, na mpango ulikuwa mzuri;
1: Wingbacks wake kuwakabia juu fullbacks wa Yanga (pin them back)
2: Watatu wa juu na kuzuia utatu wa Yanga kwenye kuanzisha mashambulizi (Job + Bacca na Aucho)
3: Na mistari miwili ya chini kuubana uwanja juu ili kuwalazimisha Yanga hasa Diarra kupiga mipira mirefu . Shida kwa Azam ilikuwa nini?
Ukizuia kwa Back 3 hakikisha beki wako wa kati kati ya wale watatu wa nyuma hayupo " square " sana na wenzako yani kwenye mstari mmoja kwasababu ukifanya hivyo inahitajika pasi moja tu ya juu kuwapa shida na Diarra alifanya hivyo mara kadhaa na hapo ndio onyo likaonekana.
Yanga walianza kutatua swali la Back 3 kwa kuwasogeza Boka na Yao juu sana ili Pacome Maxi na Aziz kucheza ndani zaidi ( Maxi na Pacome hasa hasa kwenye halfspaces ) na hii ikaanza kutengeneza "sintofahamu" kwa Back 3 ya Azam.
Baada ya Dabo kubadilisha mfumo kurudi na Back 4 ambayo ikawa inamuhitaji Adolp kushuka katikati ya mabeki wawili ilikuwa too late, maana Yanga wakaifunga mechi kabisa, wanazuia kwa idadi kubwa ya wachezaji, utulivu, matumizi ya nguvu kwenye maeneo sahihi na wakati sahihi.
GAME OVER
NOTE
1: Fei atafunga magoli tu ndio utaratibu wake
2. Ile pasi ya Mudathir
3: Boka ni Powerful Unit, anatafuna uwanja kwa spidi sana
4: Pacome dribbling zake, zina shida kwa wapinzani
5: Mzize dhidi ya waliochoka, anakwaza nguvu kasi
6: Job + Bacca ishazoeleka
7: MAXI anakula nini? Hachoki?
FT: Yanga SC 4-1 Azam FC.