Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kumuenzi Hayati Magufuli kwa Style hii...!

Yanga Magufuli Viongozi wa Idara ya Habari ya Yanga

Wed, 16 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Primia Ligi) 2021/2022, Timu ya Yanga imepanga kuadhimisha tukio la kumbu kumbu cha Kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati John Pombe Magufuli kwa kutoa misaada kwa watu wenye uhitaji.

Rais Magufuli ambae alifariki Dunia Machi 17, 2021, siku ya kesho anatimiza mwaka mmoja hivyo kwa utaratibu wa Klabu hiyo wameona wafanye jambo katika maadhimisho ya hayo.

Katika Mkutano na Waandishi wa Habari leo Machi 16, Viongozi wa Idara ya Habari wa Yanga wameelza lengo kuu kama Klabu kuelekea siku hiyo,

"Sisi Klabu Yanga, Viongozi, benchi la ufundi, wachezaji kwa namna uongozi utakavyoamua tutakwenda katika Hospitali ya Ocean Road Jijini Dar es Salaam ikiwa kama sehemu ya utamaduni wetu chini ya GSM Foundation kutoa sapoti yetu na kile tulichojaliwa kwa watu wenye uhitaji" amesema Manara

Chanzo: www.tanzaniaweb.live