Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

West Ham kuipelekaa FA mahakamani

Lucas Paqueta To City Lucas Paquetá

Fri, 26 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mabosi wa West Ham United wanafikiria kukipeleka mahakamani Chama cha Soka England (FA) baada ya kuona kuna uwezekano kiungo Lucas Paqueta akafungiwa maisha kujihusisha na soka kutokana na madai ya kuhusika katika masuala ya kubeti.

Inaelezwa kwamba Paqueta anakabiliwa na tuhuma za kufanya faulo kwa makusudi katika michezo ya Ligi Kuu England ili apate kadi za njano dhidi ya Leicester, Aston Villa, Leeds na Bournemouth ambapo kuna uwezekano mkubwa akafungiwa maisha ikiwa atakutwa na hatia.

Kwa sasa Paqueta, 26, anaruhusiwa kuichezea West Ham United hadi mchakato na hukumu itakapotoka na hadi sasa supastaa huyo amekana kuhusika na tuhuma hizo.

Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, West Ham United inafikiria kwenda kwenye Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) huko Lausanne ili kuzuia FA kusikiliza na kutoa hukumu katika kesi hiyo.

The Sun linadai timu hiyo inatilia shaka mamlaka ya FA kuhusu suala hilo na inaamini litakuwa ni jambo lisilo na maana kwa staa huyo kupewa adhabu ya kufungiwa maisha.

Kiungo huyo kwa mara ya kwanza alituhumiwa kujihusisha na masuala ya kubeti Agosti, mwaka jana, jambo lililosababisha uhamisho wake wa kutua Manchester City ufeli.

Kwa mujibu wa kanuni za FA mchezaji anayekutwa na kosa kama hilo anaweza kupewa adhabu ya kufungiwa kucheza soka miezi sita hadi maisha.

Inaelezwa wasiwasi wa West Ham United kwamba, staa huyo atafungiwa maisha umetokana na ripoti za hivi karibuni zinazoeleza kwamba katika hati ya mashtaka ya FA kuna pendekezo kwamba kikutwa na hatia afungiwe maisha.

Baada ya kukana kosa hilo, Paqueta alisema: “Nimeshangaa sana na nimekasirishwa kwa kitendo cha FA kunifungulia mashtaka. Kwa muda wa miezi tisa nimeshirikiana na kila hatua ya uchunguzi na kutoa taarifa zote walizotaka. Ninakana mashtaka yote na nitapigania hadi pumzi yangu ya mwisho kusafisha jina langu.”

Chanzo: Mwanaspoti