Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawili wanaswa na meno ya tembo Katavi

Meno Ya Tembo Wawili wanaswa na meno ya tembo Katavi

Fri, 11 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu wawili wamekamatwa wakiwa na meno mawili ya tembo katika kijiji cha Itenka Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Februari 11, 2022 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, ACP Ally Makame amesema Jeshi hilo liliwakamata watu hao wakiwa wamebeba meno hayo kwenye pikipiki ndani ya mfuko.

Amewataja watu hao kuwa ni Beno Msimbe (68) mkazi wa Ibindi na Nova Mazembe (45) mkazi wa Itenka.

"Walikamatwa Februari 10, 2022 mchana katika kijiji cha Itenka A, upelelezi unaendelea ukikamilika watafikishwa mahakamani," amesema Kamanda Makame.

Katika tukio lingine, mtu mmoja ametelekeza baiskeli yake aliyokuwa akiendesha akiwa amebeba mzigo uliokuwa na silaha aina ya gobole na nyama ya nyati kilo 60.

"Baada ya kufanyiwa upekuzi mzigo huo ulikutwa na vitu hivyo na mtuhumiwa alikimbilia porini," amesema Makame.

Advertisement Kamanda Makame ametoa onyo kwa watu wanaojihusisha na vitendo hivyo kuacha akisema Jeshi hilo limejipanga kuwasaka, kuwakamata na kuwawajibisha kwa mujibu wa sheria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live