Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawili mbaroni kwa madai ya kuua, mmoja akimtuhumu mkewe kuchepuka

Mtaki Kurwijila .png Wawili mbaroni kwa madai ya kuua, mmoja akimtuhumu mkewe kuchepuka

Thu, 12 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za mauaji katika matukio mawili tofauti ambapo watuhumiwa hao, kila mmoja alitumia kipande cha mti kumshambulia mwenzake na kusababisha kifo chake.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Septemba 12, 2024, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Mtaki Kurwijila amesema watu hao walipigwa na vipande vya mti, hivyo kujeruhiwa na kusababisha vifo vyao.

Amesema wanamshikilia Ally Abrahamu (43), mkazi wa Kijiji cha Mbangalambuyuni kilichopo Wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara ambaye Agosti 22, 2024 alimshambulia mke wake, Catherine Chinave (69) akimtuhumu kumsaliti kwa kuwa na uhusiano na wanaume wengine.

Amesema Abrahamu alianza kumshambulia mke wake kwa maneno kisha akachukua kipande cha mti na kumpiga nacho wakiwa njiani kuelekea nyumbani, wakitokea kwenye kilabu cha pombe, wakati wa usiku na kumjeruhi sehemu mbalimbali za mwili wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live