Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vinicius Jr akataa ofa ya mabilioni ya pesa kwenda Saudia

Vinicius Jr  . Vinicius Jr akataa ofa ya mabilioni ya pesa kwenda Saudia

Mon, 12 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji nyota wa Real Madrid, Mbrazil Vinicius Junior, ameripotiwa kukataa ofa ya kitita kikubwa cha pesa kutoka kwa waarabu, ili akacheze Ligi Kuu ya Saudi Arabia.

Zimekuwa zikifanyika juhudi kubwa kuhakikisha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 anacheza Saudia akiungana na mreno Christiano Ronaldo, hata hivyo Real Madrid haitaki kumuuza mchezaji huyo ambaye kifungu chake cha kuachiliwa ni Euro Bilioni moja na ana mkataba na klabu hiyo hadi mwaka 2027.

Mapema mwaka huu, Vinicius Jr alitangaza nia yake ya kuendelea kuichezea Madrid licha ya kuimbiwa nyimbo za kibaguzi kutoka kwa mashabiki wa timu pinzani.

Alisema: “Sijawahi kufikiria kuondoka LaLiga kwa sababu vinginevyo nitawapa wabaguzi kile wanachotaka.

“Nitaendelea kuwa kwenye klabu bora zaidi duniani, nikifunga mabao mengi ili waendelee kuniona. Wabaguzi wa rangi ni wachache.” alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live