Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vigogo Atletico Madrid watua kwa Gallagher

Skysports Gallagher Chelsea 6419366 Vigogo Atletico Madrid watua kwa Gallagher

Fri, 26 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Atletico Madrid ina matumaini makubwa ya kuipata saini ya kiungo wa Chelsea na England, Conor Gallagher, 24, dirisha hili.

Gallagher ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwakani, amekuwa akihusishwa kuondoka Chelsea tangu dirisha lililopita la majira ya kiangazi.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, Gallagher hana kabisa mpango wa kuondoka kwa sababu anaamini bado kuna nafasi yake Chelsea.

Kabla ya Atletico, mara kadhaa Tottenham ilidaiwa kutaka kumsajili kiungo huyu lakini iliangukia pua kutokana na mchezaji mwenyewe kutokuwa tayari.

Fundi huyu ambaye pia ni nahodha, msimu uliopita alikuwa katika orodha ya mastaa walioonyesha kiwango bora katika kikosi cha kwanza cha Chelsea.

Wakati huo huo Chelsea inataka kupunguza bei ya straika wao Romelu Lukaku kutoka Euro 44 milioni hadi 35 milioni na amekuwa akihusishwa na Napoli na timu nyingine zinazotaka kumsajili dirisha hili la usajili.

Hata hivyo, Napoli inataka kutoa chini ya Euro 25 milioni. Lukaku mwenyewe anatamani sana kujiunga na Napoli kwa ajili ya kuungana na kocha wake wa zamani, Antonio Conte lakini pia ametoa sharti la kutojiunga nao hadi pale watakapomuuza Victor Osimhen.

CRYSTAL Palace ipo katika mazungumzo na Marseille kwa ajili ya kumsajili winga wa timu hiyo na Senegal, Ismaila Sarr, 26, dirisha hili. Palace inahitaji kumsajili Sarr kwa ajili ya kuboresha eneo lao la ushambuliaji lililokuwa na mapungufu tangu msimu uliopita. Mkataba wa Sarr unamalizika mwaka 2028.

INTER Milan inaombea Arsenal ifanikiwe katika mchakato wa kumsajili beki wa Bologna na Italia, Riccardo Calafiori, 22, ili ikubali kuwauzia beki wao Jakub Kiwior dirisha hili. Arsenal inadaiwa kuwa na nafasi kubwa ya kumpata Calafiori kwa sababu imeshafanya naye hadi makubaliano binafsi. Mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.

MANCHESTER United inataka kumsajili kiungo wa Sporting Lisbon na Denmark, Morten Hjulmand, 25, ambaye katika mkataba wake kuna kipengele kinachomwezesha kuondoka ikiwa timu inayomhitaji italipa Euro 80 milioni. Staa huyu aliivutia Man United pia kutokana na kiwango bora alichoonyesha katika michuano ya Euro mwaka huu akiwa na Denmark.

MABOSI wa Chelsea wamefikia patamu katika mazungumzo yao na Villarreal kwa ajili ya kumsajili kipa wa timu hiyo na Denmark, Filip Jorgensen dirisha hili. Mbali ya Chelsea, staa huyu pia anawindwa na Marseille inayojaribu kupindua dili lake na kumsajili. Chelsea imewasilisha ofa ya zaidi ya Pauni 17 milioni. Mkataba wa Filip unamalizika mwaka 2029.

RAIS wa Real Sociedad, Jokin Aperribay ameweka wazi hadi sasa hawajaanza mazungumzo na Liverpool au timu yoyote inayohitaji saini ya winga wao kutoka Japan, Takefusa Kubo, 23, dirisha hili. Takefusa amekuwa akihusishwa sana na Liverpool inayodaiwa kutaka kumsajili kwa dau litakalomfanya kuwa mchezaji ghali zaidi kutoka Japan.

NEWCASTLE United ipo kwenye hatua za mwisho kukamilisha dili la beki wa AC Milan, Mjerumani Malick Thiaw, 22, kwa dau linalodaiwa kufikia Pauni 35 milioni.

Thiaw mwenyewe ameonyesha nia ya kutaka kutua Newcastle na amependezwa na ofa ambayo amewekewa mezani na mabosi wa timu hiyo. Msimu uliopita Thiaw alicheza mechi 30 za michuano yote.

Chanzo: Mwanaspoti