Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Video: Maamuzi ya teknolojia ya VAR yazua gumzo mchezo wa Spurs Vs Rochdake AFC

Video Archive
Wed, 7 Mar 2018 Chanzo: bongo5.com

Klabu ya Totteham Hotspur usiku wa jana imefanikiwa kuchomoza na ushindi mnono wa mabao 6 – 1 dhidi ya Rochdake AFC na kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la FA.



Kubwa lililozua gumzo katika mchezo huo wa jana usiku ni juu ya maamuzi ya teknolojia ya video ‘assistant referee’ (VAR) ambayo yameshuhudia magoli kadhaa kukataliwa na magoli mengine yakiwa yenye utata zaidi wakati Spurs wakishuhudia penati ya Son ikikataliwa na baadhi ya mabao mengine.



Hata hivyo straika wa Spurs, Fernando Llorente kwa mara ya kwanza ameipatia timu yake mabao matatu‘hat-trick’ katika dakika ya (47’,53 na 59) wakati wengine waliyotupia akiwa ni Son(23 na 65) na Walker-Peters (90+3).

Kama isingekuwa msaada wa kiteknolojia ya video ‘assistant referee’ (VAR) basi Son angefanikiwa kupiga‘hat-trick’ baada ya hiyo penati yake kukataliwa.



Licha ya kutumika kwa mfumo huo mpya wa teknolojia moja ya kivutio kikubwa ni hali ya hewa ya baridi iliyokuwa ikionekana katika dimba hilo la Wembley.

Chanzo: bongo5.com