Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Yanga yatua Mwanza bila Zahera

Video Archive
Sun, 7 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Yanga imetua Mwanza asubuhi ya leo Jumamosi kwa ajili ya mchezo wake wa Ligi Kuu dhidi ya African Lyon unaotarajiwa kupigwa Jumatatu katika uwanja wa Kirumba. Kikosi hicho kimewasili na msafara wa watu 26 ikiwa wachezaji 22 na viongozi wanne,huku Kocha Mkuu,

Mwinyi Zahera akikosekana katika kundi hilo. Meneja wa timu hiyo,Hafidh Swalehe amesema makosa yaliyoonekana katika mechi iliyopita dhidi ya Ndanda hawatarajii kujirudia badala yake wanatarajia ushindi.

Ameongeza kuwa wanajua wazi Lyon wanahitaji pointi tatu ili kujikwamua mkiani, hivyo watakuwa makini sana kuwakabili ili kufikia malengo yao.

Yanga imetua jijini hapa majira ya saa 1:30 asubuhi na Shirika la Ndege ya Air Tanzania na kupokelewa na mashabiki wake ambao waliwasindikiza kutoka uwanja wa ndege hadi mjini. Mwisho....



Chanzo: mwananchi.co.tz