Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Tazama Luis Miquissone alivyoanza mazoezi na Simba

Video Archive
Thu, 27 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Luis Miquissone, jana Julai 26, 2023 alianza rasmi mazoezi ya uwanjani siku chache baada ya kutangazwa kusajiliwa Simba akitokea Al Ahly ya Misri.

Miquissone ambaye amerejea kwa mara nyingine ndani ya Simba baada ya awali kuuzwa kwa Al Ahly, alionekana akikimbia uwanjani huko nchini Uturuki ambako wameweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi 2023-24.

Kabla ya kuuzwa, Luis alikuwa kipenzi cha mashabiki wa Simba baada ya kuonesha uwezo mkubwa katika Ligi na mashindano ya Kimataifa hususan pale alipowatungua goli Al Ahly kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live