Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Upinzani wasaini makubaliano kushirikiana na Museveni

Museveni Uchumi Upinzani wasaini makubaliano kushirikiana na Museveni

Thu, 21 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda na mgombeaji mara mbili wa urais, Nobert Mao ametia saini makubaliano ya ushirikiano na chama tawala cha National Resistance Movement kufuatia mkutano na Rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni katika Ikulu ya Entebbe siku ya Jumatano.

Museveni alituma video fupi ya kutiwa saini kwa makubaliano hayo kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Aliwasifu viongozi wa Chama cha Democratic kwa kile alichotaja kuwa ni ishara ya ukomavu, mtazamo wa mbele na siasa za kujenga.

Mao amekuwa rais wa chama cha Democratic tangu 2010 na alianza kuonekana katika siasa za kitaifa mwaka 1996 alipochaguliwa kuwa mbunge ambapo alihudumu kwa mihula miwili.

Alijitokeza kwa ufasaha wake na msimamo wake wa kupinga.

Chama chake kimekumbwa na migawanyiko ya ndani kwa miaka kadhaa.

Kabla ya uchaguzi wa 2021, alipoteza viongozi kadhaa katika chama chake na kujiunga na National Unity Platform cha Bobi Wine.

Wafuasi wa Mao wataona maendeleo haya kama ushirikiano mzuri wa vyama viwili lakini wale wanaompinga watahisi kuwa anatoa lawama kwa shutuma zao za awali alizotoa kwa Museveni.

Wakati huo huo Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametetea uamuzi wa serikali yake wa kutotoa ruzuku au kupunguza ushuru akisema pesa hizo zingetumika kutatua shida zinazoikabili nchi.

Alikuwa akihutubia taifa katika hotuba iliyorushwa kwenye televisheni Jumatano usiku huku kukiwa na ongezeko kubwa la kupanda kwa gharama za maisha kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta na uhaba wa chakula katika baadhi ya maeneo nchini.

Rais Museveni alisema ruzuku inawapotosha watu kufikiri kwamba kuna mengi na wanashindwa kujipanga kiuchumi kwa kile walichonacho na hatimaye kumaliza akiba ya kigeni ya nchi.

Alisema kupunguzwa kwa ushuru pia kutasababisha kukwama kwa miradi ya miundombinu.

Rais Museveni alituma video ya kusaini makubaliano na Democratic Party kwenye Twitter

Chanzo: www.tanzaniaweb.live