Tume ya Uchaguzi ya Uganda imeanza kutoa matokeo ya awali yanayoonesha kuwa Rais aliyeko madarakani, Yoweri Museveni anaongoza dhidi ya mpinzani wake wa karibu Robert Chagulanyi 'Bobi Wine'.
Kwa mujibu wa BBC Swahili, tayari tume hiyo imeanza kutoa matokeo ya awali leo, Ijumaa, kutoka vituo 330 vya kupigia kura. yanayoonesha Museveni anaongoza katika mbio za kukitetea kiti chake kwa muhula wa sita.
Nchi hiyo katika uchaguzi wa mwaka huu imeweka jumla ya vituo 34,684 vya kupigia kura nchi nzima.
Mwenyekiti wa Tume hiyo Simon Byakamba amenukuliwa akisema: “Hatutumii mtandao wa ndani kusambaza matokeo bali tunatumia mfumo wetu, wananchi wasijali matokeo yatatoka tu licha ya kwamba mtandao umefungwa.”