Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Trent kujazwa noti abaki Liver

Trent Arnold Mpunga Trent kujazwa noti abaki Liver

Thu, 25 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Liverpool inajiandaa kumpa Trent Alexander-Arnold ofa nono ili asaini mkataba mpya wa kuendelea kubaki Anfiled wakati beki huyo akijiandaa kuipiga chini Real Madrid inayowania saini yake.

Mapema mwezi huu, ilifahamika kwamba beki huyo wa kulia wa Liverpool ameivutia miamba ya Hispania, Real Madrid na inapanga kumsajili katika dirisha hili la uhamisho la majira ya kiangazi.

Kutokana na ukweli kwamba Alexander-Arnold ameingia katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake, haikushangaza kuona kwamba Real Madrid imefufua mipango ya kumhitaji.

Hata hivyo, ripoti zinadai beki huyo amedhamiria kubaki Anfield na kwamba klabu hiyo inajiandaa kumpa ofa ya mkataba mpya wa muda mrefu.

Kwa mujibu wa The Sun, Alexander-Arnold amezungumza na kocha mpya Arne Slot na amedhamiria kubaki katika zama mpya za Mholanzi huyo Merseyside baada ya kuondoka kwa Jurgen Klopp.

Chanzo kilisema: “Trent ameshazungumza na kocha mpya tayari. Hii ilifanyika kabla ya michuano ya Euro na wanaendelea kuwasiliana.

“Walikuwa na mazungumzo mazuri awali, lakini kocha aliheshimu kwamba alihitaji kuweka akili yake katika michuano (Euro).”

Kufikia sasa, Alexander-Arnold amecheza mechi 310 akiwa na Liverpool, akifunga mabao 19 katika michuano yote.

Pia ameshinda taji la Ligi Kuu England, Ligi ya Mabingwa Ulaya, Kombe la FA na Carabao Cup mara mbili, akiwa na klabu hiyo ya Merseyside. Ameitumikia timu yake ya taifa ya England katika mechi 29.

Chanzo: Mwanaspoti