Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tariq asaini mmoja Prisons, aweka vita nzito kwa mastraika

Tariq Simba Prisons Tariq Simba

Sat, 13 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati dirisha la usajili likitarajia kufungwa Jumatatu Januari 15, Tanzania Prisons imeendelea kujiimarisha kwa kumsainisha mkataba straika Tariq Simba aliyekuwa Geita Gold.

Hadi sasa timu hiyo haijaweka wazi wachezaji walioachwa wala kuingia kwa kipindi hiki cha dirisha dogo, lakini Mwanaspoti inafahamu Tariq anakuwa mchezaji wa tano kutua kikosini humo.

Straika huyo aliyesaini mwaka mmoja anaungana na wenzake wapya Ally Msengi, Feisal Simkoko, Abdulkarim Segeja na Jacob Benedict huku uongozi ukieleza kutangaza rasmi dirisha litakapofungwa.

Kutua kwa nyota huyo wa zamani wa Polisi Tanzania kunaifanya safu ya ushambuliaji kufikisha wachezaji nane wakiwa ni Samson Mbangula, Jeremia Juma, Messi Roland (Cameroon) Mambote Assis (DR Congo), Msengi, Benedict, Segeja na kuweka vita nzito ya namba kikosini.

Ofisa habari wa timu hiyo, Chacha Waisaka amesema wanaendelea kuisuka timu hiyo kuhakikisha ligi inaporejea wanaendeleza moto wao.

Amesema hadi sasa bado usajili unaendelea kutokana na mahitaji ya timu akibainisha kuwa iwapo watakamilisha wataweka wazi kujua nani katoka au kuingia.

"Kwa maana hiyo tuwe wavumilivu hadi uongozi utakapokamilisha usajili, kwa sababu mazungu yapo kwa wachezaji waliopendekezwa na mambo yakiwa tayari tutaweka wazi" amesema Waisaka.

Hata hivyo Maafande hao muda wowote wanatarajia kutimkia Kiwira huko Tukuyu kwa ajili ya kambi ya muda kabla ya kurejea jijini hapa tayari kwa Ligi Kuu mwezi Februari.

Chanzo: Mwanaspoti