Dar es Salaam. Baraza la Uongozi la Chama cha Mawakili Tanzania Bara (TLS) limezitaka mamlaka zilizopewa nguvu ya kuwachukulia hatua mawakili kuwasikiliza kabla ya kuwachukulia hatua.
SOMA ZAIDI: Fatma Karume adai hukumu kuzuia wakurugenzi kusimamia uchaguzi ni kuzuia goli la mkono
Taarifa ya Baraza hilo iliyotolewa jana Septemba 26, 2019 imesema “Baraza la Uongozi linawataarifu wale waliopewa mamlaka ya kuwaonya na kuwasimamisha mawakili kuwapa haki ya kusikilizwa kabla ya kuwapa adhabu kali ya kusimamishwa au kuondolewa kabisa kwenye uwakili” imesema taarifa ya Baraza hilo iliyosainiwa na Rais wa Chama cha Mawakili Tanzania Bara (TLS), Dk. Rugemeleza Nshalla.
SOMA ZAIDI: Fatma Karume asimamishwa uwakili, mwenyewe asema ataendelea kupambana
Taarifa hiyo imesema kuwa sheria ya chama hicho inampa mamlaka Jaji Mkuu au Jaji yoyote wa Mahakama Kuu kumuonya au kumsimamisha wakili yoyote lakini kumsimamisha wakili bila kumpa haki ya kusikilizwa ni kivunja sheria.
Baraza la uongozi la TLS limetoa taarifa yake siku Saba baada ya Rais mstaafu wa Chama hicho Fatma Karume kusimamishwa uwakili.
Pia Soma
- Maisha ya pacha kijijini mwaka mmoja baada ya kutenganishwa
- Watumia jina la Askofu Ruwa’ichi kutapeli wananchi
- ‘Mahabusu wa Lugola’ apandishwa kizimbani, arudishwa mahabusu
SOMA ZAIDI: Fatma Karume: Natafakari kuingia kwenye siasa