SERIKALI ya Sudan imekataa kuletwa kwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa uliokusudia kufanya tathmini ya vita vinavyoendelea nchini humo na kutafuta suluhisho la kuwalinda raia dhidi ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Uamuzi huu umetokana na hali ambapo kikosi cha kijeshi cha RSF na vikosi vya waasi kuendelea kupigana huku ukiukwaji wa haki za binadamu ukiendelea kufanyika.
Kiongozi wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa, Chande Othman, alisema: “Kutokana na kushindwa kwa pande zote zinazopigana kutafuta muafaka wa kumaliza vita, ni muhimu vikosi huru vipelekwe ili kutafuta suluhisho.”
Ujumbe huo pia uliomba vikwazo vya silaha kuwekwa kwa pande zote zinazohusika katika mapigano hayo.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan imesema kwamba serikali imekataa mapendekezo ya ujio wa ujumbe wa kutafuta ukweli wa vita.
Mpaka sasa, maelfu ya watu wamepoteza maisha na zaidi ya milioni nane wamekimbia makazi yao kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan.