Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Siri nzito utekaji Dar na maeneo mengine ya nchi

MBOWE ApLS9.jpeg Freeman Mbowe

Fri, 23 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, ameibua tuhuma nzito dhidi ya kikosi maalum cha utekaji kinachoongozwa na Zonal Crime Officer (ZCO) ACP Faustin Mafwele, akidai kwamba kikosi hicho kinahusika na utekaji na mauaji ya watu nje ya utaratibu rasmi.

Akizungumza na wanahabari Agosti 22, 2024, jijini Dar es Salaam, Mbowe alidai kuwa baadhi ya watu waliouawa walitelekezwa kwenye pori la Katavi, maarufu kwa fisi wenye uwezo wa kutafuna mifupa kama biskuti.

Mbowe pia alitaja majina ya watu waliokamatwa na kikosi hicho, akiwemo Sativa, Soka, Mlay, na Mbise, akisisitiza kwamba Mwenyezi Mungu alimuokoa Sativa kutoka kifo kwa miujiza. Matamshi haya yanakuja wakati ambapo suala la utekaji na mauaji linaendelea kuzua mjadala mkubwa nchini.

“Kama Chama tumechunguza kutoka vyanzo vyetu vya ndani na vingine vya ndani ya Jeshi la Polisi na Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama, nitaeleza kwa kifupi tulichogundua na tunaowaonyooshea vidole ili Polisi na hao wengine watusute watuambie Mbowe mnasema uongo, uchunguzi wetu unatupeleka wapi?

"Moja kuna kitu kwenye Kanda Maalum ya Dar es saalam kinaitwa Task Force ya Ulinzi na Usalama, Task Force hii iliundwa ikishirikisha Wadau kutoka Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa na hata JWTZ, katika hatua ya baadaye Jeshi la Wananchi liliondoka katika oparesheni hii.

"Na Task Force hii ilipoundwa kwa mara ya kwanza iliundwa kama Kikosi maalum cha kupambana na wizi ambacho kinasimamiwa na ZCO ambaye sasa hivi anayeongoza Ofisi hiyo anaitwa ASP Faustin Mafwele huyu ndio Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalum ya Dar es salaam ambaye anasimamia Kikosi hiki.

“Oparesheni centre ya kikosi hiki ipo nyuma ya Kituo cha Polisi Chang’ombe na mtambue Kikosi hiki hakiingiliwi na mfumo wa kawaida wa utawala wa Polisi kwahiyo hakifanyi kazi ndani ya Vituo vya Polisi, nyuma ya Kituo cha Polisi cha Chang’ombe kuna kambi ya Kikosi hiki na imezungushiwa uzio wa mabanzi pale ndani wanateswa Watu, wanaumizwa Watu, wanafinywa Watu pale ndio mateso ya Watanzania wanapopitia.

“Kwa taarifa tulizonazo kwa mwaka huu na sehemu ya mwaka jana, wapo Watanzania zaidi ya 200 hawajulikani walipo na mambo haya ni mwendelezo wa maelekezo ya Viongozi wa Serikali ambao huko nyuma walipaswa kusema shughulikeni nao.

“Sisi kama Chama tumesema tuyaseme haya kwa sauti ili yasikike zaidi, utekaji huu umeambatana na mauaji, awali waliokuwa wanauawa kienyeji walikuwa wanapelekwa mochwari, wengine kama Sativa walipelekwa pori la Katavi wakaliwe na Fisi kwasababu wanasema Katavi ndio pori lenye Fisi wakali ambao hata mfupa wanautafuna kama biskuti, Mungu hakupenda akamwokoa, Sativa alikamatwa na kikosi hiki na Mafwele anajua na kikosi hiki ndicho kimemkamata Soka, Mlay na Mbise,” amesema Mbowe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: