Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida Fountain Gate yafungiwa kusajili na FIFA

Thabo Senong..png Singida Fountain Gate yafungiwa kusajili na FIFA

Fri, 26 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Fountain Gate zamani Singida Fountain Gate FC imefungiwa kufanya usajili mpaka itakapomlipa aliyekuwa kocha wake Thabo Senong.

Taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) leo Julai 26, 2026 imeeleza kuwa, uamuzi huo umefanywa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) baada ya kocha huyo kushinda kesi ya madai dhidi ya klabu hiyo.

Senong raia wa Aftika Kusini alifungua kesi FIFA akidai malipo ya malimbikizo ya mishahara, na fidia ya kuvunjiwa mkataba kinyume na taratibu.

Fountain Gate ilitakiwa iwe imemlipa kocha huyo ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo ulipotolewa, lakini haikutekeleza hukumu hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live