Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simbachawene amaliza utata uraia wa Kibu

567f5c03e9779245f494f44be1df9605 Simbachawene amaliza utata uraia wa Kibu

Mon, 4 Oct 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amemaliza mgogoro wa uraia wa mshambuliaji mpya wa Simba, Kibu Denis ambaye aliwahi kuchezea Mbeya City kabla ya kutua Msimbazi.

Hivi karibuni iliripotiwa kuwa, Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Kim Paulsen alishindwa kumjumuisha Kibu katika kikosi chake kutokana na kushindwa kutambulika uraia wake.

Baada ya sakata hilo, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imejitokeza na kutoa ufanunuzi, ambapo sasa Kibu amepewa uraia wa Tanzania ambapo aliwahi pia kucheza Taifa Stars.

“Kwa mamlaka aliyopewa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, kwa mujibu wa Sheria ya Uraia, Sura ya 357 (Rejeo la 2002), baada ya kupokea ombi lililoletwa na TFF, nimempa uraia wa Tanzania mchezaji wa mpira wa miguu, Kibu Denis Prosper Septemba 30, 2021,” taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani ilisema kupitia kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii.

Simbachawene alisema uraia wa asili wa Kibu alikuwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), lakini amekuwepo Tanzania tangu mwaka 1998 akiwa na umri wa miaka sita baada ya wazazi wake kukimbia machafuko ya kisiasa nchini humo.

Alisema mchezaji huyo ana nyaraka zinazoonesha ni raia wa Tanzania ikiwamo kitambulisho cha uraia, kwani alikuwa anajijua ni Mtanzania kutokana na kuingia nchini akiwa na umri mdogo na hana historia yoyote na nchi yake ya asili zaidi ya kukulia Tanzania.

Kibu alicheza mchezo wa kirafiki Julai 13, 2021 kati ya Taifa Stars na Malawi ambapo Stars waliondoka na ushindi wa bao 2-0 katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Chanzo: www.habarileo.co.tz