Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba Queens yasepa na 24, Mgunda afafanua ishu ya Mnunka

Mgunda X Simba Queens Simba Queens yasepa na 24, Mgunda afafanua ishu ya Mnunka

Wed, 14 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha Mkuu wa Simba Queens, Juma Mgunda amesema kikosi hicho kitasafiri leo kwenda Addis Ababa, Ethiopia kwa ajili ya kushiriki michuano ya Klabu kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) kwa wanawake.

Michuano hiyo kwa msimu huu itafanyika Ethiopia kuanzia Agosti 17 hadi Septemba 4, 2024 na bingwa atakata tiketi ya kushiriki fainali za Klabu Bingwa Afrika, ambayo Simba ilishiriki mara ya kwanza 2022 na kumaliza nafasi ya nne, huku msimu uliopita ilienda JKT Tanzania ambayo ilitolewa hatua ya makundi.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mgunda amesema jana walifanya mazoezi ya mwisho kabla ya kuanza safari na baadhi ya wachezaji waliokuwa majeruhi wamepona.

Ameongeza, jioni ya leo anatarajia kuondoka na kikosi cha wachezaji 25 ambao wamesajiliwa na Simba akiwemo Aisha Mnunka ambaye Mwanaspoti iliripoti, ametoroka kambini ingawa kocha huyo hakufafanua kwamba amerudi au la akisema muda wa kuliongelea hilo litafika.

"Tunashukuru kambi imekwenda vizuri na tukiamka salama leo tunaanza safari tukiwa na wachezaji 25 ambao wamesajiliwa na timu na tunaamini tutakwenda kufanya vizuri," amesema Mgunda na kuongeza;

"Mnunka ni moja ya wachezaji tuliowajumuisha na kwa sasa sio muda mzuri wa kuzungumzia hilo lakini fahamuni kuwa tuko vizuri na jana tulikaa na viongozi wakazungumza na wachezaji kuwapa hamasa na tunawashukuru kwa kutimiza matakwa ya benchgi la ufundi kwa kusajili watu tuliowataka."

Simba ambayo imeangukia Kundi B ikiwa pamoja na PVP Buyenzi ya Burundi, Kawempe Muslim Ladies ya Uganda na FAD ya Djibouti.

Agosti 18 itaanza kuminyana na FAD, Agosti 21 dhidi ya Kawempe kisha kufunga hesabu na PVP Agosti 24 kwenye hatua ya makundi.

Chanzo: Mwanaspoti