Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Siku ya Mwananchi; Gamondi uso kwa uso na Mokwena

Mokwena Gamondi Mz Siku ya Mwananchi; Gamondi uso kwa uso na Mokwena

Wed, 24 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuelekea kilele cha siku ya Mwananchi tayari Yanga SC walishaanza maandalizi ya ndani na nje ya uwanja ili kufanikisha na kuhakikisha kuwa tukio hilo linafana, na miongoni mwa maandalizi yaliyofanyika ni pamoja na kumtafuta mpinzani watakae kutana nae kunako kilele cha sherehe hizo.

TAARIFA ZA AWALI Yanga SC waliwatumia barua ya mualiko Wydad AC ya Morocco na maridhiano yalikuwa vizuri ila mbeleni Wydad AC wakapata ratiba zingine za maandalizi yao ya msimu mpya hivyo wakaiweka pembeni ratiba ya mechi dhidi ya Yanga SC kunako Mwananchi Day.

Yanga SC walikua na machaguo ya timu zingine tayari endapo Wydad AC wasingeridhia na miongoni mwa machaguo yao ni kutokea Afrika mashariki,Africa ya kati,Kaskazini na Kusini mwa Afrika.

KWA SASA HALI IKO HIVI Wydad AC baada ya kumpata kocha mpya 'Rhulani Mokwena' na kuanza kazi ya kupitia mafaili ndipo ikaonekana kuna mechi ambayo kwa timu zote mbili inaweza kuwaongezea kitu kikubwa kiufundi, hivyo kwa sasa tayari Wydad AC wamefufua matamanio ya kutaka kucheza tena na Yanga SC kunako kilele cha Siku ya Mwananchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live