Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samatta ana ugomvi na Kocha Amrouche?

Video Archive
Thu, 18 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kufanyiwa mabadiliko dakika ya 69 na nafasi yake kuchukuliwa na kiungo Feisal Salum 'Fei Toto', nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Mbwana Ally Samatta alitoka moja kwa moja na alionekana kutokupeana mkono na Kocha wake Adel Amrouche kitendo kilichojadiliwa kuwa kuna sintofahamu baina yao.

Akizungumzia hilo baada ya mchezo huo kumalizika na Stars kuchabangwa bao 3-0 dhidi ya Morocco, Samatta ameweka wazi kuwa hana ugomvi na kocha huyo raia wa Algeria na kwamba kila kitu kipo sawa

"Hakuna shida mimi na kocha, kwenye camp tuko pamoja wala stars haijagawanyika," amesema Samatta.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live