Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samatta, Msuva watemwa Taifa Stars, Job arejea (+Video)

Video Archive
Mon, 26 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa Tanzania Hemed Seleman ‘Moroco’ amewatema baadhi ya mastaa wa kikosi hicho, huku akimrejesha kikosini mlinzi Dickson Job.

Stars inayotarajiwa kuingia kambini keshokutwa inajiandaa na michezo miwili ya kutafuta nafasi ya kufuzu Mataifa Afrika 2025 itakayochezwa nchini Morocco.

Katika kikosi hicho kilichoitwa kocha Moroco hajawaita wachezaji Kelvin John ‘Mbappe’ nahodha wa kikosi Mbwana Samatta na, Simon Msuva wanaocheza soka lao ughaibuni.

Samatta na Msuva wametemwa kikosini huku beki Dikson Job akirudishwa baada ya kuwapo na tetesi za kuwa na sintofahamu na kocha huyo.

Morocco alitolea ufafanuzi ishu ya Job akisema, "Mimi na Job tumezungumza yameisha salama."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live