Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rekodi za Spurs London zashtua, mabosi matumbo joto

Ange Postecoglou At Tottenham Rekodi za Spurs London zashtua, mabosi matumbo joto

Wed, 18 Sep 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Rekodi za Tottenham Hotspur dhidi ya mahasimu wake wa jadi wa London tangu wawe chini ya Kocha Ange Postecoglou imekuwa ya ovyo zaidi baada ya kipigo kingine kutoka kwa Arsenal, Jumapili iliyopita.

Spurs ilichapwa 1-0 nyumbani licha ya Arsenal kukosa mastaa kibao kwenye kikosi chao cha kwanza. Declan Rice, Martin Odegaard, Mikel Merino na Oleksandr Zinchenko ni miongoni mwa wachezaji wa Arsenal ambao walikosa mechi hiyo.

Kikosi cha Arsenal chini ya Kocha Mikel Arteta kilipambana na kupata ushindi, shukrani kwa bao la kichwa la beki Gabriel Magalhaes kwenye kipindi cha pili, liliofanya Spurs kuchapwa na sasa ikishika nafasi ya 13 kwenye msimamo, ikiwa na pointi nne tu katika mechi nne.

Sasa, Spurs imepoteza mechi mbili mfululizo baada ya kuchapwa 2-1 na Newcastle United kabla ya mapumziko ya mechi za kimataifa.

Na mashabiki wa Spurs sasa wameanza kupata wasiwasi kutokana na rekodi za mechi dhidi ya wapinzani wao muhimu wa London tangu walipoanza kuwa chini ya Postecoglou. Licha ya kukabiliana na timu nyingine za London kama Brentford, Crystal Palace na Fulham, mashabiki wa Spurs wao wanaodhani mahasimu wao wa jadi ni Arsenal, Chelsea na West Ham United.

Lakini, Postecoglou alipotua kwenye kikosi hicho majira ya kiangazi 2023, hajawahi kushinda mechi yoyote dhidi ya wapinzani hao. Kwenye mechi saba alizocheza chini ya mahasimu hao, sare ni mbili tu na vilivyobaki vyote ni vichapo.

REKODI ZA SPURS DHIDI YA WAPINZANI WA JADI CHINI YA KOCHA ANGE

-Septemba 2023 vs Arsenal 2-2

-Novemba 2023 vs Chelsea 4-1

-Desemba 2023 vs West Ham 2-1

-Aprili 2024 vs West Ham 1-1

-Aprili 2024 vs Arsenal 3-2

-Mei 2024 vs Chelsea 2-0

-Septemba 2024 vs Arsenal 1-0

*Mechi 7, ushindi 0, sare 2, vichapo 5

Chanzo: Mwanaspoti