Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais wa Marekani, akemea jaribio la mauaji ya Trump

Rais Wa Marekani, Akemea Jaribio La Mauaji Ya Trump.png Rais wa Marekani, akemea jaribio la mauaji ya Trump

Tue, 17 Sep 2024 Chanzo: Voa

Rais wa Marekani, Joe Biden, amekemea jaribio la pili la mauaji dhidi ya mtangulizi wake, na kulaani ghasia hizo za kisiasa kuwa sio tabia za Marekani.

“Hakuna mahali kwa kufanya vurugu za kisiasa Marekani,” Rais Biden aliuambia mkutano wa vyuo vikuu na vyuo vikuu vya watu Weusi (HBCU), akiwa mjini Philadelphia, Jumatatu.

Amesema ndani ya Marekani, kuna usuluhishaji wa tofauti zetu kwa amani kwa kutumia sanduku la kura, lakini sio wa mtutu wa bunduki. Rais Biden amesisitiza kwamba Marekani iliteseka mara nyingi na mikasa ya mauaji ya bunduki na kwamba njia hiyo haisuluhishi chochote zaidi ya kusambaratisha nchi.

Maoni ya Biden yametolewa takriban saa 24 baada ya maafisa wa idara ya ulinzi wa viongozi ya Marekani, kumwona mtu anayeshukiwa kuwa na bunduki kwenye uwanja wa gofu wa Rais mstaafu Donald Trump, West Palm Beach, Florida.

Chanzo: Voa