Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Museveni kumualika Rais Macron wa Ufaransa

Macron Museveni Command One Post Rais Museveni kumualika Rais Macron wa Ufaransa

Thu, 20 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amesema anapanga kumualika rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron kuzungumza namna ya kumaliza mgogoro na nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Museveni ameandika “Nimekutana na balozi wa Ufaransa anayemaliza muda wake [Uganda], Jules-Armand Aniambossou aliyenieleza mambo mbalimbali ambayo Ufaransa inashughulikia ikiwemo kutafuta amani ya kudumu kaskazini kwa DRC.”

“Nitamuandikia [Bwana] Macron na kumualika aje tujadili kuhusu masuala ya Afrika na dunia ikiwemo Ulaya”. Museveni amemwambia balozi Aniambossou wakati wa mkutano wao Jumatatu jioni.

“Ninatamani sana kuketi nae na kuzungumza kimkakati na Macron. Ulaya haina cha kupoteza ikifanya kazi vizuri na Afrika”.

DRC inakabiliana na waasi wa M23 kwenye upande wa kaskazini wa nchi hiyo huku waasi hao wakitajwa kulishinda jeshi la DRC na kutwaa mji wa kimkakati wa mpakani na baadhi ya maeneo karibu na jimbo la Kivu Kaskazini.

Mwezi uliopita wakati wa mkutano wa Umoja wa Mataifa, rais Macron alikutana na rais wa DRC Felix Tshisekedi na hasimu wake Paul Kagame kwa ajili ya mazungumzo ya amani kufuatia wawili hao kutuhumiana kwneye mkutano huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live