Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Museveni atishia kuondoa majeshi ya Uganda nchini Somalia

Museveni7777 Yoweri Museveni, Rais wa Uganda

Thu, 9 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametishia kuyaondoa majeshi ya nchi yake katika mpango wa usalama nchini Somalia.

Licha ya kwamba sio mara ya kwanza kwa Rais huyo kutishia, amekuwa akifanya hivyo baada ya viongozi wa nchi hiyo kuhatarisha amani ya nchi hiyo na mpango wa uchaguzi unaopangwa kufanyika.

Akizungumza na chombo cha habari cha Ufaransa ‘France 24’ Rais Museveni amejibu swali aliloulizwa kuhusu mpango wake wa kuondoa majeshi yake ya UPDF nchini Somalia baada ya ongezeko la mashambulizi kutoka kwenye kundi la waasi la Al-Shabab pamoja na mgogoro wa kisiasa nchini humo.

Akielezea mgogoro wa kisiasa nchini Somalia mwaka 2011, Museveni alitaka maelewano ambayo yalipelekea kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu kipindi hicho Mohamed Abdullahi Farmaajo ambaye kwa sasa anahudumu kama Rais na katika kipindi hicho Museveni alitishia kuondoa majeshi yake.

Uganda inakuwa nchi ya kwanza kupeleka majeshi yake nchini Somalia kupitia mwamvuli wa kulinda amani Afrika wa mwaka 2007.

Wakati huo, Al-Qaeda wakishirikiana na Al-Shabaab walitishia kuiondoa madarakani serikali iliyokuwa ikungwa mkono na mataifa ya Magharibi. Wiki chache baadae, Uganda ilituma jeshi lake baada ya Azimio la Umoja wa Mataifa lililofanyika mwezi Machi, kuusaidia Umoja wa Afrika nchini Somalia hadi Disemba mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live