Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameitisha mkutano wa viongozi wa Afrika Mashariki kuzungumzia vita ya wenyewe kwa wenyewe inayoendelea nchini Ethiopia.
Taarifa hii imetolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya nchini Uganda, na kubainisha kuwa Rais Museven anafanya mawasiliano na Waziri Mkuu wa nchini Ethiopia kuhusu yanayoendelea nchini humo.
"Rais Museveni anawasiliana na waziri mkuu wa Ethiopia, Abiy [Ahmed] kuhusu hali inayoendelea Ethiopia na ameelezea wasiwasi juu ya kundi la waasi la Tigray kukataa kufanya majadiliano ili kusitisha mapigano," Okello Oryem alinukuliwa.
Mkutano huo umeitishwa Novemba 16, na Tayari mjumbe maalum kutoka Marekani amefika Ethiopia kujadili mgogoro huo.