Tue, 13 Aug 2024
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Rasmi Kipa Ayoub Lakred hatokuwa sehemu ya kikosi cha Simba katika msimu ujao, baada ya Viongozi kupendekezwa akatwe katika usajili ili nafasi yake achukue mshambuliaji Mcameroon, Lionel Iteba.
Simba imepanga kuiboresha safu ya ushambuliaji ya timu hiyo, kwa kumsajili Iteba ili aje kusaidiana na Steven Mukwala alisajiliwa hivi karibuni.
Muda wowote Simba inatarajiwa kumalizana na mshambuliaji sambamba na kumtangaza baada ya kufikia makubaliano mazuri ya pande ya Menejimenti ya Iteba na Simba.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live