Usilolijua ni kwamba kuna mastaa wa soka wanaofanya vizuri ndani ya Yanga na huwezi kuwakosa kwenye kikosi cha kwanza katika mechi muhimu, lakini wako pamoja hadi nje ya uwanja.
Sio wengine ni Yao Kouassi, Pacome ZouZoua wote hawa kutokea nje ya nchi lakini wanafanya vizuri sana katika timu yao.
Iko hivi; ukaribu wao sio ndani ya kikosi tu kumbe hadi kupanga wanakaa nyumba za karibu, ila kubwa zaidi wananyolewa na kinyozi mmoja.
Aloo hawa watu unaambiwa nje ya uwanja ni watu poa sana kwa mujibu wa kinyozi wao anayejulikana kwa jina la Msukuma.
Ingawa watu hawawezi kufanana, ila hawa wanaendana karibu kila kitu,kinyozi huyo akizungumza na Mwanaspoti kuipa hali halisi ya maisha ya wachezaji hawa nje ya uwanja.
Amesema kuwa kwa upande wa Yao ni mtu mkimya asiye na mambo mengi yaani kijana flani hivi moyo safi, lakini pia sio mbabaifu linapokuja suala la mkwanja hanaga kabisa mambo ya kupunguza bei.
Mwingine anayetajwa kuwa karibu nao, Msukuma amesema ni mtu poa pia muda mwingi hupendelea kucheka, lakini anapenda kuchongwa vizuri nywele na kuweka rangi nyeusi tofauti na Pacome.
Pacome ndiye chanzo. Msukuma anasema Pacome ni chanzo cha yeye kufahamiana na hawa wote japokuwa hawanyoi wachezaji hao tu.
“Wakati naenda kumnyoa Pacome ndio alinikutanisha na wengine ijapo siwanyoi muda mmoja au siku moja, lakini mimi ndio kinyozi wao,” anasema Msukuma.
“Muda mwingi nawanyoa mchana wakitoka mazoezini kabla hawajaenda mapumziko. Wote hawana shida na hata hawa wawili wananilipa vizuri tu kama anavyofanya Pacome."
Unataka kufahamu supastaa gani mwingine wa Yanga na tabia zake na anayewekwa sawa kimuonekano na Msukuma?