Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndoto ya Kariakoo iliyokamilika Singida

Ade Singisda Ndoto ya Kariakoo iliyokamilika Singida

Mon, 16 Sep 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Miaka ya hivi karibuni, klabu ya Arsenal Uingereza imekuwa na tabia moja isiyoeleweka pale dirisha la usajili linapofunguliwa.

Kwa mara kadhaa imekuwa ikihusishwa na usajili wa wachezaji tofauti tofauti lakini mwisho wa siku haiwapati na mastaa hao kwenda kwingineko.

Mfano ni viungo Mykhailo Mudryk, Joao Felix na Moises Caicedo ambao awali walihitajika na kutajwa sana kujiunga na Arsenal lakini baadae wote wakanyakuliwa na Chelsea.

Ni kawaida kwenye soka na kuna matukio mengi ya namna hiyo. Hapo ndipo soka linanoga zaidi kwani halijawahi kutabirika.

Toka England njoo moja kwa moja hadi Tanzania. Huku unakutana na Ligi Kuu. Ligi pendwa zaidi ukanda wa Afrika Mashariki na kati lakini pia ligi inayokua kwa kasi.

Huku nako 'mambo na vijimambo' ya namna hiyo yapo sana na leo gazeti hili litakupa mkasa wa Mshambuliaji Victorien Adebayor raia wa Niger aliyezaliwa mwaka 1996.

Adebayor kwa sasa ni mchezaji wa Singida Black Star aliyojiunga nayo katika dirisha kubwa la usajili akitokea Association sportive de la Garde nationale nigerienne maarufu kama AS GNN ya nchini kwao.

Staa huyo anayemudu kucheza winga zote mbili sambamba na mshambuliaji ws kati ni miongoni mwa majina yaliyoimbwa sana katika vipindi vya usajili na mapacha wa katiakoo Simba na Yanga lakini ghafra tutamuona kwenye jezi za Singida.

Jina la Adebayor lilianza kugonga vichwa vya habari nchini mwaka 2022 baada ya kuonekana akiwa na kikosi cha Union Sportive de la Gendarmerie Nationale maarufu USGN ya Niger kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.

Ilikiwa ni kwenye mechi za hatua ya Makundi ambapo timu yake hiyo ilikutana na Simba na kufungwa 4-0 uwanja wa Mkapa kutoa sare ya mabao 1-1 nchini Niger. Hapo ndipo Simba na Yanga zilimuona na kuanza kumfuatilia kwa ukaribu.

Simba na Yanga zilivutiwa na Staa huyo na kutaka kumsajili katika dirisha la usajili lililofuata lakini ziligonga mwamba.

Wakati mbio za kupata saini yake zikiendelea, Yanga ilijitoa na Simba ikabaki kidedea lakini nayo mwisho wa siku ilishindwa kumnasa kutokana na kuzidiwa dau na waarabu RS Berkane waliomvuta kwao.

Simba kumkosa Adebayor iliumia kama iliumia sana na baadhi ya mashabiki wa Msimbazi waliwalalamikia viongozi wa timu hiyo kwa uzembe.

Hata hivyo Staa huyo akiwa Berkane aloshindwa kupata muda wa kutosha kucheza. Simba ikapata taarifa na kuanza kumnyemelea lakini ilimkosa tena kwani baada ya kuvunjiwa mkataba na Berkane alijiunga na Amazulu ya Afrika Kusini msimu wa 2023/2024.

Dirisha dogo la msimu huo Simba ikarejea tena kwa Adebayor lakini ikamkosa kwa mara nyingine kwani alijiunga na AS GNN ya nchini kwao.

Msimu huu Simba ilimuhitaji tena Staa huyo lakini kutokana na mabadiliko ya usajili na sera mpya ya yimu hiyo ya kusajili wachezaji vijana, basi ikaachana naye na Adebayor akajikuta akitua Singida.

Tayari ametambulishwa Singida lakini hajaichezea mechi hata moja timu hiyo kutokana na kuchelewa kujiunga na kikosi hicho kinachonolewa na Patrick Aussems.

Siku chache zilizopita alikuwa kwenye kikosi cha timu yake ya Taifa, Niger kilichokua ugenini kucheza na Libya na baada ya mechi za kitaifa atarejea Singida.

Wale mashabiki wa Simba na Yanga waliokuwa wakitamani Adebayor azichezee timu zao za Kariakoo watamuona kwenye ligi akiwa na Singida kwa sasa labda hadi hapo baadae mambo yakibadilika.

DONDOO ZA ADEBAYOR

Licha ya kuwa na ubora mkubwa lakini Adebayor ni miongoni mwa wachezaji ambao hawana sifa ya kucheza kwenye timu moja kwa muda mrefu.

Tangu ameanza soka la ushindani msimu wa 2012/ 2013 amecheza kwenye jumla ya timu 13 tofauti ikiiwa ni wastani wa timu moja kila msimu.

Msimu wa 2019/2020 akiwa Ghana nyota yake ilianza kung'aa zaidi kwani aliibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu nchini humo akifunga mabao 12.

Msimu wa wa 2021/2022 ambapo Simba na Yanga zilianza kumtolea macho akifunga mabao sita kwenye Kombe la Shirikisho Afrika na msimu uliopita akiwa kwa Niger aliubuka mfunga bora wa ligi hiyo akifunga jumla ya mabao 29 kwenye michuano yote.

Aidha alichaguliwa kuwa MVP wa Niger kwa msimu uliopita.

Chanzo: Mwanaspoti