Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#NBCLIGIREVIEW: Tazama magoli yote Kagera Sugar vs Simba (+Video)

Video Archive
Thu, 22 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeji Kagera Sugar wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Ni Kagera Sugar ya kocha Mecky Mexime iliyotangulia kwa bao la Deus Bukenya dakika ya 15, kabla ya beki Mkongo, Henock Inonga Baka kuisawazishia Simba dakika ya 38.

Kwa matokeo hayo, Kagera Sugar wanafikisha pointi 23 na kusogea nafasi ya sita, wakati Simba inayofikisha pointi 38 inabaki nafasi ya pili baada ya wote kucheza mechi 17.

Ni mabingwa watetezi, Yanga SC wanaoendelea kuongoza Ligi Kuu baada ya raundi 17, wakiwa na pointi zao 44, wakati Azam FC yenye pointi 37 ni ya tatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live