Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#NBCLIGIREVIEW: Tazama goli la Yanga katika mchezo Vs Geita Gold FC (+Video)

Video Archive
Mon, 7 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Timu ya Yanga jioni ya Jana ilikuwa kule katika Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza wakikipiga na Geita Gold.

Mchezo huo wa Ligi Kuu Bara (NBC Primia Ligi)2021/2022 ulitamatika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa goli 1-0.

Goli hilo la pekee na la ushindi la Yanga limefungwa na Mshambuliaji Fiston Mayele sekunde ya 30 tu tangu kuanza kwa mchezo huo.

Ushindi huo wa jana unazidi kuiweka Yanga katika mazingira mazuri ya kunyakua taji la Ligi Kuu msimu huu, kwa kuwaweka kileleni huku wakifikisha alama 45 wakitofautiana alama 11 na wanaokamata nafasi ya pili Simba SC wenye alama 34 japokuwa Simba wana mchezo mmoja mkononi.

Tanzania Web tunakusogezea matukio yote muhimu yaliyojitokeza katika mchezo huo, kwa kutazama video fupi ambayo tumekuwekea hapa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live