Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzize hajawahi kufunga mabao ya kuibeba timu - Oscar Oscar

Clement Mzize Tinhoooo Mzize hajawahi kufunga mabao ya kuibeba timu - Oscar Oscar

Thu, 12 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuhusu ubora wa mshambuliaji wa Yanga na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Clement Mzize umekuwa na dosari kwa upande wa mchambuzi wa michezo Oscar Oscar ambaye alisema kwamba, mchezaji huyo licha ya kufunga mabao lakini hajawahi kufunga mabao ya kuibeba timu.

“Huu ni msimu wa tatu tunamshuhudia Mzize. Ni mchezaji mzuri sana, lakini hajawahi kufunga hata mabao 10 ya ligi. Hajawahi kufunga mabao ya kuibeba timu kwenye mazingira magumu na hana mabao mengi yanayokumbukwa na wengi.

“Natamani tungeacha mchezo wa kuongeza sifuri. Natamani tungeacha mchezo wa Waingereza. Mzize bado ni mchezaji ambaye kwenye nafasi tano anaweza kufunga bao moja. Bado anakua.”

“Kuna watu wameanza kumpa jina na la Didier Drogba. Ni vizuri mtu kuwa na ndoto kubwa, lakini ni vizuri zaidi kuwa na ndoto zenye uhalisia. Tuna kijana anaitwa Kelvin John. Ni Mtanzania mwenzetu. Ni kijana wetu na anacheza Ligi Kuu Denmark. Wakati anaanza kuchipukia alipewa jina la Mbappe. Hadi leo hakuna mfanano wowote,” amesema Oscar Oscar.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live