Tue, 13 Aug 2024
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Mzee, Juma Ally Magoma na Geofrey Mwaipopo, wamekamatwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kughushi saini za wajumbe wa baraza la wadhamini wa Yanga.
Wakili wa mzee Juma Magoma na Mwaipopo, Jacob Masenene, amesema kuwa, kosa walilokamatiwa wateja wake linadhaminika, amekamilisha taratibu zote za kupata dhamana ili awatoe mahabusu.
Magoma na Mwaipopo wamekamatwa leo baada ya kutoka Mahakama Kuu, kusikiliza rufaa kesi yao dhidi ya bodi ya wadhamini wa Yanga, ambayo imeahirishwa hadi Agosti 21.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: