Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mvua kubwa na mafuriko yawaua watu kadhaa kusini mwa Morocco

Watu 132 Wafariki Mwaka Huu Nchini Sudan Kutokana Na Mafuriko.png Mvua kubwa na mafuriko yawaua watu kadhaa kusini mwa Morocco

Mon, 9 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mvua kubwa ya radi na mafuriko yamesababisha takriban watu kumi na mmoja kupoteza maisha na tisa kutoweka tangu siku ya Ijumaa kusini mwa Morocco. mfumo huu wa hali ya hewa pia umeathiri nchi jirani ya Algeria, ambapo watu wawili walisombwa na mafuriko walikuwa wakitafutwa siku ya Jumapili jioni.

Hali ya hewa "ya kipekee" inaathiri Morocco. Mvua kubwa iliyoambatana na mafuriko imesababisha angalau vifo kumi na moja tangu siku ya Ijumaa Septemba 6 katika majimbo 17 na mikoa ya Morocco, ambayo baadhi yake ni nusu kame.

Kwa undani, hali mbaya ya hewa imesababisha vifo kumi na moja, ikiwa ni pamoja na saba katika jimbo la Tata, kilomita 740 kusini-mashariki mwa Rabat, vifo viwili huko Tiznit (kusini-magharibi) na vifo viwili huko Errachidia (kusini-mashariki), ikiwa ni pamoja na raia mmoja wa kigeni ambaye hajatajwa. , amebainisha msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Rachi El Khalfi, kulingana na ripoti ya muda.

Aidha, watu tisa haajulikao waliko katika maeneo ya Tata, Errachidia na Taroudant (kusini-magharibi).

"Kiwango cha mvua kilichorekodiwa kwa siku mbili ni sawa na kile kilichotokea katika mikoa hii kwa kawaida katika mwaka mzima," msemaji wa wizara amesema. Pia ametangaza kubomoka kwa nyumba 40 nchi nzima na uharibifu wa barabara 93, pamoja na mitambo ya maji, umeme na mawasiliano.

Nchini Algeria, hali ya mvua kubwa ya vurugu kama hiyo ilikumba maeneo ya jangwa kama Sahara, kulingana na picha zilizorushwa kwenye mitandao ya kijamii.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live