Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Musiba apigwa faini bil.7.5 kesi ya Fatma Karume

Musiba Cyprian Musiba

Wed, 11 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama Kuu ya Zanzibar, leo August 11 imemtia hatiani Bw.Cyprian Musiba na gazeti lake la Tanzanite kwa kosa la kumchafua (defamation) Wakili Fatma Karume kwa kumzushia taarifa za uongo zenye lengo la kushusha hadhi yake katika jamii.

Katika hukumu hiyo Musiba ametakiwa kumlipa Fatma kiasi cha shilingi bilioni 7.5 Bilioni kama fidia ya hasara aliyoipata baada ya kuchafuliwa na maneno hayo.

Wakili Fatma, kupitia mitandao ya kijamii ameonesha kufurahishwa na maamuzi ya Mahakama kuhusu kesi hiyo huku akimtaka Mwanaharakti huyo kumlipa fidia hiyo haraka iwezekanavyo.

Kesi hiyo iliyofunguliwa Septemba 28 mwaka 2019, katika Mahakama Kuu Zanzibar, mara baada ya Musiba kupitia gazeti lake la Tanzanite kuchapisha habari iliyomuhusu Wakili huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live