Mgombea wa urais wa Uganda kupitia chama cha ‘National Resistance Movement’ Yoweri Museveni ametangazwa kuwa mshindi wa nafasi hiyo baada ya kupata kura 5,851,037 ambazo sawa na 58.64% ya kura zote zilizopigwa.
VIDEO >>> Museveni vs Bobi Wine: Mambo matatu kuhusu Uchaguzi Mkuu Uganda
Mpinzani mkuu wa Museveni katika kinyang’anyiro hicho Robert Kyagulanyi maarufu kama ‘Bob Wine’ ameshika nafasi ya pili kwa idadi ya kura 3,475,398 sawa na 34.83% ya kura zote zilizopigwa.
Uganda ilifanya uchaguzi Alhamisi tarehe 14, Januari 2021 na umefikia tamati hii leo mara baada ya Museveni kutangwaza mshindi wa kiti cha urais.
Ushindi huo unamaanisha kuwa Museveni ataendelea kuliongoza Taifa la Uganda kwa muhula mwingine baada ya kukaa madarakani kwa miaka 35.