Kampala. Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameongeza siku 21 za wananchi kukaa ndani kuanzia kesho Aprili 15 hadi Mei 5, 2020 baada ya siku 14 za kwanza kumalizika leo lengo likiwa ni kujikinga na maambuziki ya corona. Ameongeza kuwa wameongeza siku 21 baada ya kuwepo kwa mafanikio kwa muda wiki tatu tangu kuanza kutangazwa uamuzi hayo. Museveni amesema suala la usafiri wa umma litajadiliwa na kupendekeza usafiri wa baiskeli kwa sababu unabeba mtu mmoja na ni wa afya. Amesema kabla ya ugonjwa huo kuingia asilimia 40 ya watu walikuwa wanakufa hospitali kwasababu ya kula sana na kutofanya mazoezi kwa hiyo baiskeli zitasaidia.