Chama tawala nchini Uganda, NRM kimefanya maadhimisho ya siku ya vuguvugu na ukombozi huku Rais Yoweri Museveni akitimiza miaka 37, madarakani.
Sherehe hizo, zimefanyika katika Wilaya ya Kikumiro iliyopo katikati mwa nchi ambapo Museveni pia aliorodhesha mafanikio kadhaa ambayo Waganda wanajivunia ikiwemo suala la kukomesha ukabila na migawanyiko ya kidini.
Aidha, Wakosoaji wa Serikali wakiwemo viongozi wa upinzani ambao waliwahi kushiriki katika utawala wake, wamemtaka Museveni kuchana na ajenda ya azimio lao la kuikomboa Uganda dhidi ya utawala duni.
Hata hivyo, baadhi yao wamesema wanakubali kwamba Museveni amefanya juhudi katika kuboresha uthabiti wa usalama, lakini bado zipo chagamoto katika masuala ya kupambana na ufisadi na kuwainua Waganda kiuchumi.