Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Museveni, Ruto na Odinga wakutana Uganda

Museveni, Ruto Na Odinga Wakutana Uganda Museveni, Ruto na Odinga wakutana Uganda

Tue, 27 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni na Rais wa Kenya William Ruto pamoja na kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga wamechapisha picha wakiwa pamoja katika mtandao wa X, (Zamani Twitter).

Watatu hao wamekutana jana nchini Uganda katika shamba la Rais Museveni lililoko huko Kisozi ambapo mbali na kujadili diplomasia, wamezungumzia pia hatua ya Odinga kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika.

“Nilifurahi kukutana na Rais Ruto na Odinga mchana huu katika shamba langu la Kisozi. Tulijadili masuala yenye maslahi kati ya nchi zetu mbili na Jumuiya ya Afrika Mashariki. Ninawakaribisha,” ameandika Museveni kwenye X.

Naye, Rais Ruto amesema ana furaha ya kukutana na Rais Museveni nyumbani kwake. Wamejadili masuala muhimu yanayoathiri nchi zao hizo kama vile nishati na petroli.

“Katika mkutano wangu na Rais Museveni leo, pia tulijadili haja ya nchi hizi mbili kufuatilia kwa haraka usanifu na ujenzi wa bomba la bidhaa iliyosafishwa ya mafuta ya petroli Eldoret-Kampala-Kigali,” ameandika.

Ameongeza kuwa Kenya na Uganda zimejitolea kuimarisha uhusiano wa muda mrefu wa kidiplomasia na kiuchumi. Uhusiano huo ni pamoja na kuleta mataifa yote saba ya Jumuiya ya Afrika Mashariki karibu katika lengo lao kuu la kuunda shirikisho la kisiasa la Afrika Mashariki.

Ruto ameongeza kwamba: “Pia kilichojadiliwa ni Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya, Raila Odinga kutangaza kugombea uenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika.”

Kwa upande wake, Odinga amesema: “Siku kadhaa zilizopita, nilikubali mwaliko kutoka kwa Rais Museveni kwa mkutano wa pamoja na Rais Ruto leo kujadili kuimarika kwa utangamano wa kikanda ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.’’

Pia, ameongeza kuwa walijadili kuhusu kugombea kwake Uenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika.

“Ninamshukuru sana Rais Museveni kwa kuidhinisha kwa dhati kuteuliwa kwangu na kwa Rais Ruto kuniunga mkono kikamilifu.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live