Luanda, Angola. Marais Paul Kagame (Rwanda) na Yoweri Museveni (Uganda) wamesaini makubaliano ya kubadilishana wafungwa.
Makubaliano hayo yamekuja muda mfupi baada ya mazungumzo ya upatanishi yaliyoongozwa na Serikali ya Angola.
Mazungumzo hayo yalifanyika jana Jumapili Februari 3 mjini Luanda.
Hata hivyo, hakukuwa na taarifa zaidi kuhusu idadi ya wafungwa watakaohusika katika mpango huo wala muda wa kuachiwa kwao.
Kagame na Museveni waliwahi kuwa washirika wakubwa kabla hawajaingia katika mgogoro huku kila nchi ikiituhumu nyingine kuendesha ujasusi dhidi yake na kuyasaidia makundi yenye lengo la kuangusha serikali zao.
Katika mkutano wa jana ambao ulimshirikisha pia Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Felix Tshisekedi viongozi hao walikubaliana kukutana tena Februari 21, kwenye mpaka wa Gatuna.
Pia Soma
- Mbatia, Musukuma wataka Mtume Mwamposa kujadiliwa bungeni
- Katiba ya Tanzania yatajwa kikwazo uraia pacha
- Wagonjwa wa corona wafikia 10 Ujerumani
- Somalia yatangaza hali ya dharura
Agosti mwaka jana nchi hizo zilisaini makubaliano ya kuboresha uhusiano wa kisiasa na wa kibiashara lakini hakukuwa na maendeleo ya maana.