Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muhoozi asema atatuma wanajeshi kumlinda Putin

Muhoozi Kainerugaba Putin Muhoozi Kainerugaba na Putin

Fri, 31 Mar 2023 Chanzo: VoA

Mtoto wa kiume wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Muhoozi Kainerugaba jana Alhamisi alitangaza kwamba nchi yake itatuma wanajeshi kuulinda mji wa Moscow ikiwa utakabiliwa na tishio.

“Niite mfuasi wa Putin ukipenda, lakini sisi, Uganda tutatuma wanajeshi kuilinda Moscow ikiwa itatishiwa na mabeberu, “Muhoozi Kainerugaba alisema kwenye Twitter.

Jenerali huyo wa jeshi ambaye ni mfwasi mkubwa wa Rais wa Russia Vladimir Putin ameongeza kuwa “ Nchi za magharibi zinapoteza muda wake na propaganda zisizo na maana za kuiunga mkono Ukraine.”

Kainerugaba ambaye amepata umaarufu mkubwa kwenye mtandao wa Twitter kutokana na maoni yake kuhusu masuala mbalimbali, mapema mwezi huu alitangaza kwamba anapanga kuwania urais kwenye uchaguzi wa 2026.

Jana, alitangaza pia kuwa ataanzisha kituo cha televisheni na radio chini ya chapa yake ya MK, na amesema mmoja ya maeneo ya kwanza atakayotembelea itakuwa Russia.

Chanzo: VoA