Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muhoozi: EAC tukingane Museveni awe Rais

Museveni Uchumi EAC tukingane Museveni awe Rais

Tue, 4 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamanda wa Jeshi la Ardhini la Uganda Muhoozi Kainerugaba ambaye ni Mtoto wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni, amesema kama dhamira yake ya kuifanya Afrika Mashariki kuwa Taifa moja ikikamilika, Baba yake Rais Museveni atakuwa ndiye Rais wa Muungano huo.

Muhoozi amesema”Tukiungana na kuwa Taifa moja, Museveni atakuwa Rais, Ruto atakuwa Makamu wa Rais, Uhuru Kenyatta atakuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Mimi Muhoozi nitakuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF) wa Muungano wa Afrika Mashariki.

Muhoozi amesema hayo baada ya kuandika kupitia twitter kwamba amekutana na Baba yake (Rais Museveni) na kumueleza kwamba Vijana wa Afrika Mashariki wameamua Nchi za Afrika Mashariki ziungane na kuwa Taifa moja”

Muhoozi amesema mipaka iliyopo iliwekwa na Wakoloni na hakuna haja ya kuendelea kuiacha badala yake Nchi za Afrika Mashariki zinapaswa kuifuta mipaka hiyo na kutengeneza Taifa moja.

Kauli ya Muhoozi inakuja siku moja tu baada ya kuandika kwenye mtandao wa twitter kuhusu kutofurahishwa kwake na hatua ya Rais wa zamani wa Kenya, Uhuru Kenyatta kutogombea muhula wa tatu katika uchaguzi wa hivi karibuni na kusema yupo tayari yeye na Jeshi lake kuiteka Nairobi ndani ya wiki moja tu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live