Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msigwa avutiwa ubora wa Boka mechi Yanga, Azam

Msigwa Mkutanoni Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa.

Tue, 13 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa, amekunwa na kiwango kilichooneshwa na beki wa kushoto wa Yanga, Chadrack Boka, katika mchezo wa fainali wa Ngao ya Jamii 2024 dhidi ya Azam FC uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam juzi.

Msigwa hakusita kueleza kuvutiwa kwake na beki huyo, wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa mchezo huo ambao Yanga ilifanikiwa kubeba ngao hiyo kwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-1. 

"Boka ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa, hawa ndio aina ya wachezaji ambao tunawahitaji kwa ajili ya kuliboresha soka la Tanzania," alisema Msigwa akiachilia furaha yake.

Aidha, aliwataka wachezaji wa Tanzania kuiga aina ya uchezaji wake ili waweze kupata nafasi ya kwenda kucheza soka la kulipwa nje ya nchi. 

"Natamani wachezaji wetu waige aina ya uchezaji wake, ananifurahisha kwa kuwa anafahamu kile ambacho anakifanya ndani ya uwanja," alisema. 

Katika hatua nyingine aliipongeza timu ya Yanga kutokana na kuendeleza ushindani wake na kuweza kutwaa ubingwa wa Ngao ya Jamii 2024 kwa kuifunga Azam FC mabao 4-1. Boka ambaye amesajiliwa Yanga msimu huu, alianza kucheza soka katika klabu za nyumbani kabla ya kujiunga na FC Saint Eloi Lupopo ya Ligi Kuu ya DR Congo, na kuonesha uwezo mkubwa uliomfungulia milango ya kuitwa timu ya taifa.

Kwa upande wa timu ya taifa, Boka aliitwa kwa mara ya kwanza kuchezea DR Congo Agosti 28, 2022 na hadi sasa, ameicheza mechi sita.

Ametua Yanga kuchukua nafasi ya Mkongomani mwenzake, Joyce Lomalisa ambaye aliachana na Yanga baada ya mkataba wake kumalizika mwishoni mwa msimu uliomalizika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: