Jose Mourinho na timu yake ya Fenerbahçe wamesukumizwa nje ya michezo ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kufuatia kipigo cha jumla cha 3-2 dhidi ya vigogo wa Ufaransa Lille kwenye mechi ya kufuzu UCL.
Mchezo huo ulilazimika kwenda kwenye muda wa ziada kabla ya Lille iliyokuwa pungufu ya mchezaji mmoja kupata bao la kusawazisha dakika za jioni kwenye muda wa ziada.
Itakumbukwa Fenerbahçe ilipoteza 2-1 kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza kabla ya kutoka sare ya 1-1 kwenye marudiano na kuondoshwa kwa katika ya jumla ya 3-2. Fenerbahçe itacheza Ligi ya Europa msimu ujao
FT: Fenerbahçe 1-1 Lille (Agg. 2-3)
⚽ Diakite 90+1’
⚽ David (P) 116’.