Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mohamed Salah, Kevin De Bruyne wanasakwa Saudia

Salah X Kdb Hhh Mohamed Salah, Kevin De Bruyne wanasakwa Saudia

Tue, 13 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Saudi Pro League imeweka wazi mpango wao ima kumnasa Mohamed Salah au Kevin De Bruyne kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya ya kiangazi kama tu fursa hiyo itapatikana.

Baada ya kusumbua sana kwenye dirisha la majira ya kiangazi la mwaka jana, wakati timu za ligi hiyo ya Mashariki ya Kati zilipotoa pesa za maana kusajili mastaa, safari hii wamekuwa na utulivu mkubwa wakisubiri kuona kama kuna uwezekano wa kumnasa staa wanayemtaka.

Licha ya kwamba dirisha bado halijafungwa, lakini klabu za Saudi Arabia zimeonekana kushusha ile kasi yao ya kutumia pesa kwenye usajili.

Saudi Pro League timu zake zilitumia Pauni 700 milioni kwenye dirisha la mwaka jana, kiwango ambacho kilifanya ligi hiyo kuzidiwa na ligi tatu tu kwenye matumizi ya pesa za usajili, ambazo ni Ligi Kuu England, Ligue 1 na Serie A.

Katika Pauni 700 milioni, Pauni 560 milioni zilitumika kunasa mastaa waliokuwa kwenye timu za Ligi Kuu England, kuzifanya timu ya ligi hiyo nazo kuingia sokoni kunasa mastaa wapya na kuwafanya kutumia karibu Pauni 2.36 bilioni.

Mastaa wa Liverpool, Jordan Henderson na Fabinho na mastaa watatu wa Chelsea, kiungo mkabaji na Ngolo Kante, beki wa kati, Kalidou Koulibaly na kipa Edouard Mendy, ambao wote walitua zao kujiunga na klabu hizo za Mashariki ya Kati.

Lakini, uhamisho wa Moussa Diaby kutoka Aston Villa kwenda Al-Ittihad kwa ada ya Pauni 50.5 milioni unabaki kuwa uhamisho mkubwa zaidi uliofanywa na timu hizo za Saudi Pro League kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Pesa bado zipo kama klabu hizo za Saudia zitaamua kusajili. Kitengo cha usajili cha ligi hiyo kimedaiwa kimetengeneza bajeti ya miaka minane kwa ajili ya kusajili wanasoka wa kimataifa.

Na sasa miamba hiyo imetegesha ndoano yao kwa Salah na De Bruyne ambao inaweza kuwanasa bure kabisa endapo kama hawatapewa mikataba mipya. Na sasa Saudi Pro League inaweza kusubiri hadi Januari kunasa wakali hao, endapo hawatapewa dili jipya.

Usajili wa mastaa wenye majina makubwa bado umeshindwa kuongezea thamani ligi hiyo kwenye upande wa mapato ya televisheni, ambayo ni Pauni 100 milioni kwa mwaka. Ni Pauni 10 milioni hadi Pauni 15 milioni tu ndizo zilizotoka kwa watangazaji wa nje ya nchi hiyo ya Kiarabu.

Lakini, wanaamini usajili wa mastaa kama Salah na De Bruyne unaweza kubadili hali ya upepo na kuwaongezea thamani kubwa sokoni.

Chanzo: Mwanaspoti