Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkosoaji mwingine wa mamlaka ya Senegal akamatwa

Senegal Senegalllll.png Mkosoaji mwingine wa mamlaka ya Senegal akamatwa

Mon, 9 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nchini Senegal, mtu mwingine ambaye anachukuliwa kuwa mkosoaji mkubwa wa utawala wa Senegal amekamatwa kwa ombi la upande wa mashtaka, hatua ambayo imezua imezua gumzo.

Cheikhouna Keïta, mkuu wa zamani wa Kurugenzi ya Ofisi Kuu ya kukabiliana Usafirishaji Haramu wa Dawa za Kulevya na sasa kiongozi wa vuguvugu la "Force dolel Askanwi" yuko rumande. Anatuhumiwa kueneza habari za uongo kuhusu serikali.

Mamlaka yatolewa wito wa kurekebisha sheria

Kama ilivyopendekezwa na Baraza la Haki mwanzoni mwa mwezi Juni, Seydi Gassama anatoa wito kwa mamlaka kurekebisha sheria ambayo inatumika kwa aina hii ya makosa.

"Kwa makosa yote yanayohusiana na uhuru wa kujieleza ambao ndio kitovu cha mjadala wa kidemokrasia, ni lazima tuweze kuondoa vifungo vya jela. Hatuombi kuruhusu watu kutukana wengine, kukashifu wengine, lakini tunaomba vikwazo vingine, sawia zaidi vitumiwe kwa makosa haya, mjadala huo wa kidemokrasia usiwe chanzo cha wasiwasi."

Kama vile Alioune Tine wa Kituo cha Africajom, Seydi Gassama anatoa wito wa kuachiliwa mara moja kwa Cheikhouna Keïta na Ahmet Suzanne Camara, wanaozuiliwa tangu Julai 24 kwa kumtusi mkuu wa nchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live