Thu, 10 Feb 2022
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Kakwenza Rukirabashaija ambaye aliwekwa chini ya ulinzi kwa takriban mwezi mmoja akituhumiwa kumkosoa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amekimbia Nchini humo. Wakili wa Mwandishi huyo amesema mazingira yalikuwa magumu kwake kuendelea kukaa.
Mwandishi huyo aliachiwa mwishoni mwa Januari baada ya kukamatwa Desemba kwa Makosa ya Mawasiliano yanayohusiana na mfululizo wa 'Tweets' alizochapisha kuhusu Rais Museveni na Mwanaye.
Mahakama iligoma kulegeza Masharti yake ya Dhamana ikiwemo agizo la Rukirabashaija kutozungumza na Waandishi wa Habari. Pia, kumekuwepo na madai aliteswa alipokuwa anashikiliwa.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live