Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkongwe wa Riadha Tanzania, Gidabuday afariki Dunia (+Video)

Video Archive
Tue, 10 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa Katibu Mkuu Riadha, Wilhelm Gidabuday amefariki dunia saa 7 usiku wa kuamkia leo Jumanne Septemba 10, 2024 baada ya kugongwa na gari eneo la Maji ya Chai, mkoani Arusha.

Kwa mujibu wa Mjumbe wa Riadha kanda ya Mashariki, Alfredo Shahanga, kiongozi huyo amefariki baada ya kugongwa kwenye eneo hilo akiwa ameshuka kwenye gari akielekea nyumbani kwake.

“Ni kweli Gidabuday hatunaye,” amesema Shahanga kwa masikitiko huku akibainisha kuwa kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hili, Gidabuday amepoteza maisha hapo hapo baada ya kugongwa.

Gidabuday ni Mwanariadha wa zamani wa Tanzania ambae alikuwa akijitoa kwa kila hali kuhakikisha mchezo wa Riadha anasonga mbele ama kurudisha makali yake yale ya miaka ya nyuma. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live